Friday, March 6, 2015

Jina la mtoto wa kike wa miezi 9 wa Chris Brown lajulikana

Ni wiki sasa tangu kusambaa kwa habari kwamba Chris Brown ana mtoto wa kike mwenye umri wa miezi tisa (9) sasa. Lakini mwenyewe bado hajazungumzia kuhusu taarifa hizo kama ni za kweli au not.
Nia na Mwanae (anayesemekana kuwa ni mtoto wa Chris Brown)

Mtoto aliyeripotiwa kuwa ni mtoto wa msanii Chris Brown na mwanamitindo Nia amekuwa chanzo cha kuachana kwa Chris na mpenzi wake Karrueche Tran.  KT amesema hataki kujihusisha na kile anachokiita “Baby drama”.

Monday, January 26, 2015

Adam Mchomvu - Tiririka (Official Music Video)

Baada ya kufanya bonge la uzinduzi wa video yake hii ya Tiririka kwenye Vitu Flani Amazing Concert, Adam Mchomvu a.k.a AD+ ametupia video yake hiyo on Youtube!
Director wa video hiyo ni Hanscana ambaye amefanya video zingine kama Moyoni ya Navy Kenzo na WCD ya Vanessa Mdee. Itazame hapo juu.

D’Banj kuwashusha Amber Rose na Blac Chyna huko Nigeria kuhudhuria tukio hili

Sasa  Nigeria wanapata nafasi ya kuwaona live wale madada wanaotisha kwa kutwerk ambao they always break the internet kwa mambo yao wanayoyapost kwenye mitandao ya kijamii.

Hapa nawazungumzia Amber Rose na Blac Chyna. Warembo hao wanatarajia kushushwa nchini Nigeria na DBanj. Mtandao wa Bongo5 umeandika hivi:

Msanii wa Bongo Movie, Slim apandishwa kizimbani kwa madai haya

Msanii wa Bongo Movie ambaye anajulikana kwa jina maarufu la Slim amepandishwa kizimbani wiki ilopita.

Kwa mujibu wa mtandao wa Bongomovie, Msanii huyo alipandishwa kizimbani katika mahakama ya Mwanzo, Magomeni. Mtandao huo uliandika hivi:

Wednesday, January 14, 2015

Msanii kutoka Nigeria, Wizkid anatarajia kuja Tanzania mwaka huu

Mkali wa muziki kutoka Nigeria, Wiz Kid anatarajia kuja Tanzania ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kabisa. Msanii huyo anatamba kwa nyimbo zake nyiingii nzuri kama Caro, Azonto, In my Bed na zingine nyingi.
Wizkid

Kupitia tweet aliyoipost muda si mrefu, Wizkid alifunguka juu ya Tour anayotarajia kuianza mwaka huu. Moja ya nchi zitakazopata baraka ya Tour hiyo wa Wizkid ni Tanzania. Hii hapa tweet ya Wizkid na baadhi ya nchi anazotegemea kutembelea:

Diamond na Zari wanatarajia mtoto! Mwenyewe athibitisha kwa ‘style’ hii

Juzi kati Diamond alifunguka kwamba aliachana na akina Jokate, Wema Sepetu na Penny kwasababu walichoropoa mimba zake. Kitu ambacho wanadada hao walireact vibaya sana. Kokate alisema Diamond hana akili huku Penny alimmaliza kwa kusema msanii huyo hana uwezo wa kutia mimba!
Diamond na Zari

Sasa kwa mujibu wa mtandao wa Bongo5, nikaona taarifa kwamba Diamond anatarajia kuitwa baba baada ya kupost picha ya Ultrasound kwenye akaunti yake ya Instagram. Na swali ni kwamba je anatarajia kupata mtoto huyo kweli? Na atazaa na nani? Zari au mwingine?. Mtandao huo uliandika hivi: